Marekani-China

Mwanadiplomasia wa juu Marekani kukutana na rais wa China

Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani  Rex Tillerson( kushoto)akizungumza kwenye mkutano Korea Kusini March 17, 2017. REUTERS/JUNG Yeon-Je/Pool
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson( kushoto)akizungumza kwenye mkutano Korea Kusini March 17, 2017. REUTERS/JUNG Yeon-Je/Pool Reuters/路透社

Mwanadiplomasia wa juu wa Marekani Rex Tillerson yuko tayari kukutana na Rais wa China Xi Jinping leo Jumapili saa kadhaa baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la injini ya roketi yake hatua mabyo imeongeza shinikizo jipya jkwa mataifa yenye nguvu kushughulikia tishio kutoka Pyongyang.

Matangazo ya kibiashara

Vyombo vya habari vya Korea Kaskazini vimesema mapema leo Jumapili kwamba serikali hiyo iliyotengwa imefanya jaribio la injini yenye nguvu iliyopongezwa na rais Kim Jong-Un kama kuzaliwa upya kwa sekta yake ya roketi.

Xi amemwambia Tillerson kwamba yeye na Trump waboresha uhusiano wao kwa njia ya simu mwezi uliopita ili kufanya juhudi za pamoja za kuendeleza ushirikiano kati ya China na Marekani, nawanaamini kwamba wanaweza kuhakikisha uhusiano huo unasonga mbele katika mtindo wa kujenga katika zama mpya.

Akiwa njiani kuelekea Beijing, Tillerson alitembelea washirika wa Marekani Japan na Korea Kusini ambapo alisema Washington itaachana na mpango ulioshindwa wa uvumilivuwa kimkakati dhidi ya Pyongyang akiongeza kuwa jeshi la Marekani inaweza kuchukua hatua dhidi ya Korea Kaskazini.

Kauli hiyo inaashiria kutofautiana na China ambayo inapendelea diplomasia itumike dhidi ya maneno makali yenye kuidisha joto la mvutano.