MAREKANI-USALAMA

Usalama waimarishwa Ikulu ya Marekani baada ya vitisho

Eneo la usalama lililotengwa karibu na Ikulu ya White House mjini Washington, Machi 18, 2018.
Eneo la usalama lililotengwa karibu na Ikulu ya White House mjini Washington, Machi 18, 2018. SAUL LOEB / AFP

Usalama umeimarishwa katika Ikulu ya White House kufuatia kukamatwa kwa mtu ambaye alikuwa akipiga kelele aitoa vitisho katika moja ya maeno ya ukaguzi yaliyo karibu na White House, afisa mmoja wa serikali ya Marekani amesema.

Matangazo ya kibiashara

Mtu asiyejulikana alidai kuwa ana bomu katika gari lake, lakini alikamatwa mara moja na gari lake limezuiliwa, kwa mujibu wa runinga ya CNN.

Rais Donald Trump alikua alikwenda nyumbani kwake Florida mwishoni mwa wiki.

Aidha, kompyuta moja iliyo kuwa na siri nyingi za rais Donald Trump iliibiwa wiki moja iliyopita mjini New York kutoka mikononi ya mmoja wa maafisa Idara ya Ujasusi, taarifa hii ilitangaza Ijumaa Machi 18.

Kwa mujibu wa CNN, kompyuta ilikua chini ya ulinzi mkali lakini ilikua na mambo muhimu, ikiwa ni pamoja na plani za jengo la Trump Tower mjini New York, ambapo bado wanaishi mke na mtoto wa kiume wa rais wa Marekani, Melania na Barron Trump.

 Matukio haya yanatokea wiki moja baada ya kutolewa tahadhari. Mtu mmoja alikamatwa Machi 10 alkijaribu kuingia katika majengo ya Ikulu ya Marekani, na aliweza kutembea kwenye bustani za makazi ya rais kwa zaidi ya robo saa kabla ya kukamatwa.

Mwezi Septemba 2014, mpiganaji wa zamani aliyekua na maradhi ya akili alifaulu kuingia ndani ya Ikulu ya White House, akiwa na kisu mfukoni, baada ya kuruka juu ya uzio na kupita kwenye nyasi akikimbia.