HONDURAS-MEXICO-HAKI

Watatu wakutwa na hatia ya kupanga mauaji ya kumua Rais wa Honduras

Rais wa Honduras, Juan Orlando Hernández.
Rais wa Honduras, Juan Orlando Hernández. ©Reuters.

Mahakama nchini Honduras imewakuta na hatia watu watatu wanaofanya biashara ya madawa ya kulevya kwa kosa la kupanga mipango ya kumuua Rais wa nchi hiyo, Juan Orlando Hernandez baada ya uchaguzi mwaka 2014.

Matangazo ya kibiashara

Watatu hao wanashirikiana na magenge yanayojihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nchini Honduras.

Waendesha mashtaka wamesema mpango wa kumuua rais ulindaliwa na genge liitwalo de los Valle, nchini Honduras na kundi jingine la Sinaloa kutoka Mexico, ambalo linaongozwa na Joachim maarufu 'El Chapo' Guzman.

Itafahamika kwamba rais Juan Orlando Hernandez aliongoza kwa miaka kadhaa Kampeni dhidi ya makundi ya uhalifu yanayojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Watu hao watatu ambao wanasubiri hatma yao mwezi ujao wanatoka mataifa mawili tofauti, ambapo wawili ni kutoka Mexico, na mmoja kutoka nchi jirani ya Honduras.