MAREKANI-FORBES-UTAJIRI

Forbes: Bill Gates aongoza kwa utajiri, Trump ashuka

Mwanzilishi wa Microsoft, Bill Gates, achukua nafasi ya kwanza kwenye orodha ya watu tajiri zaidi duniani mwaka 2017.
Mwanzilishi wa Microsoft, Bill Gates, achukua nafasi ya kwanza kwenye orodha ya watu tajiri zaidi duniani mwaka 2017. REUTERS/Kevin Lamarque

Kwa mujibu wa jarida la la Forbes, Bill Gates, mwanzilishi wa Microsoft anaongoza kwa mara nyingine kwenye orodha yake ya watu tajiri zaidi duniani mwaka huu. Orodha hiyo imetawaliwa na mabilionea kutoka Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Jarida la Fobes linabaini kwamba mali ya Bw Gates imeongezeka hadi Dola Bilioni 86, kutoka Dola Bilioni 75.

Bill Gates anafuatwa na Warren Buffett, aliyeongeza utajiri wake kwa Dola Bilioni 14.8 hadi Dola Bilioni 75.6.

Rais wa Marekani Donald Trump, hata hivyo ameshuka nafasi 220 hadi 544 kwenye orodha ya jarida la Forbes ya matajiri na sasa ana mali ya Dola Bilioni 3.5 pekee.

Forbes imesema kushuka kwa utajiri wa Bw Trump kwa Dola Bilioni 1kulitokana na kuupungua kwa kasi ya sekta ya biashara ya ardhi na makao Marekani.

Katika orodha hiyo ya Forbes, mabilionea 183 walijipatia utajiri wao kupitia teknolojia, utajiri wao ukiwa jumla ya dola trilioni moja za Marekani.

Wengine walio kwenye 10 matajiri zaidi ni mwanzilishi wa Amazon Jeff Bezos, ambaye amepanda hadi nambari tatu utajiri wake ukiongezeka kwa kiwango cha juu zaidi kuliko wa mtu mwingine yeyote duniani.

Utajiri wa Amazon Jeff Bezos uliongezeka kwa Dola Bilioni 27.6 hadi Dola Bilioni 72.8.
Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg anachukua nafasi ya tano na mwanzilishi mwenza wa Oracle Larry Ellison yuponafasi ya saba.

Itafahamika kwamba idadi ya mabilionea (wa dola) duniani imeongezeka kwa asilimia 13 na kufikia 2, 043.