MAREKANI-TRUMP-AFYA

Trump atoa shinikizo kwa chama chake kabla ya kura muhimu

Donald Trump akutana na wabunge kutoka chama cha Republican, Machi 21, 2017 katika Washington.
Donald Trump akutana na wabunge kutoka chama cha Republican, Machi 21, 2017 katika Washington. AFP

Jumanne Machi 21, Rais wa Marekani Donald Trump ameonya wabunge na maseneta wa chama cha Republican kuwa wanaweza kupoteza wingi wao katika bunge la Congress kama watapiga kura dhidi ya mageuzi katika sekta ya afya ndani ya siku mbili.

Matangazo ya kibiashara

Kura dhidi ya mageuzi katika sekta hiyo inatishia kuweka uzito wake wote ndani ya sheria ya kwanza kubwa ya utawala wake.

Rais wa Marekani alijielekezaBungeni (Capitol ) kuhamasisha wabunge 237 kutoka chama cha Republican wa Bunge la Congress kuzingatia ahadi waliyoitoa katika kampeni ya uchaguzi ya kufuta na kubadilisha "Obamacare" wakati wa kura ya Alhamisi wiki hii.

"Kushindwa hakubaliki," amesema wakati wa mkutano wa faragha katika moja ya majengo ya Bunge, kwa mujibu wa mtu mmoja aaliyekuwepo katika mkutano huo.

Kupitishwa kwa marekebisho hayo itategemea agenda inayosalia ya chama cha Republican, ikiwa ni pamoja na kushuka kwa kiwango kikubwa cha kodi muswada wa sheria unaotarajiwa kupitishwa baadaye. Ili kushinda uchaguzi wa wabunge katikati mwa muhula wa mwezi Novemba 2018, itabidi kuonyesha matokeo thabiti kwa wapiga kura, alisema rais Trump.