MAREKANI-TRUMP-HAKI

Jaji Gorsuch: Trump hayuko juu ya sheria

Jaji Gorsuch ambaye alipendekezwa hivi karibuni na rais wa Marekani Donald Trump kujaza nafasi iliyo wazi kwenye mahakama kuu nchini Marekani alijaribu Jumanne wiki hii kuwashawishi maseneta kwamba yuko huru kwa ushawishi wowote wa kisiasa, bila hata hivyo kutoa maoni yake binafsi.

Jaji Neil Gorsuch (kushoto) asema Trump hayuko juu ya sheria, ikibidi kumuhukumu atamuhukumu.
Jaji Neil Gorsuch (kushoto) asema Trump hayuko juu ya sheria, ikibidi kumuhukumu atamuhukumu. ©REUTERS/Kevin Lamarque
Matangazo ya kibiashara

Jaji Neil Gorsuch ameapa kuwa huru kwa Mahakama ya Juu

Katika siku ya pili ya kusikilizwa kwa minajili ya kupitishwa na Baraza la Seneti, jaji Gorsuch alihakikisha kwamba hatakua na huruma wa kumhukumu yeyote yule, hata kama Rais Trump atakutwa na hatia.

"Hakuna mtu aliye juu ya sheria," alisema Jaji Gorsuch, mwenye umri wa miaka 49, ambaye alipendekezwa na Rais Donald Trump kujaza nafasi kwenye Mahakama ya Juu kukaa juu Mahakama Kuu kwa miongo.

Hata hivyo alikataa kutoa maoni yake kuhusu utata dhidi ya agizo linalohusu wahamiajil a rais wa Donald Trump kutoka chaa cha Republican, ambayo kwa sasa imesimamishwa jaji mmoja wa Marekani. "Siwezi kushiriki katika masuala ya kisiasa," alisisitiza Jaji Gorsuch.

Alipoulizwa kuhusu mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya Bw Trump kwa mahakama, Bw Gorsuch alizungumzia kwa ujumla bila kumtaja rais Trump.

"Wakati mtu yeyote anakosoa uamuzi, msimamo au nia ya jaji wa Mahakama, kwa upande wangu naona moja kwa moja kwamba inaumiza, na halileti sura nzuri," Jaji Gorsuch alisema.

Jaji Neil Gorsuch akisikilizwa mbele ya kamati ya sheria ya Seneti, Capitol Hill mjini Washington, Machi 20, 2017.
Jaji Neil Gorsuch akisikilizwa mbele ya kamati ya sheria ya Seneti, Capitol Hill mjini Washington, Machi 20, 2017. ©REUTERS/Jonathan Ernst