MAREKANI

Jaji nchini Marekani aongeza muda wa marufuku ya agizo la rais Trump kuhusu wakimbizi

Jaji wa Mahakama ya jimbo la Hawaii nchini Marekani ametangaza kuendeleza marufuku ya agizo la rais wa Donald Trump la kutaka raia wa mataifa sita ya Kiislamu kutozuru nchini hiyo.

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Carlos Barria
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi wa Jaji Watson unaamanisha kuwa rais Trump hataweza tena kuagiza kutekelezwa kwa agizo lake kwa sababu kwa sasa lipo Mahakamani.

Jaji huyo hata hivyo hajasema uamuzi huu wa kusitisha agizo hilo la rais Trump, utamalizika lini.

Uamuzi huu umewapa faraja kubwa wahamiaji kutoka mataifa hayo ya Kiislamu wanaotaka kwenda Marekani kwa sababu mbalimbali.

Wanaharakati walikwenda Mahakamani kupinga agizo la rais Trump wakisema ni la kibaguzi, linakiuka haki za binadamu lakini pia linaathiri sekta ya utalii nchini humo.

Hata hivyo, rais Trump amekuwa akisema agizo lake lililenga kuwazuia magaidi kuja nchini Marekani na ulikuwa ni uamuzi wa kiusalama.

Mataifa ambayo yalikuwa yameathiriwa na agizo la Trump ni pamoja na Iran, Syria, Libya, Somalia, Sudan na Yemen.