MAREKANI-KOREA KASKAZINI

Trump asisitiza kuwa Marekani inaweza kuishambulia Korea Kaskazini peke yake

Shambulizi la silaha za nyuklia nchini Korea Kaskazini
Shambulizi la silaha za nyuklia nchini Korea Kaskazini KNS / KCNA / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa tahadhari kwa Korea Kaskazini na kusema, nchi yake iko tayari kuishambulia hata bila ya msaada wa China.

Matangazo ya kibiashara

Onyo hili limekuja saa chache kabla ya maadhimisho ya kumbumkumbu ya kuzaliwa kwa Baba wa taifa hilo Kim Il Sung mwishoni mwa wiki hii.

Wachambuzi wa siasa na usalama wanasema kuwa huenda Pyongyang ikatumia maadhimisho hayo ya 105 kujaribu silaha zake za Nyuklia.

Trump amesema Korea Kaskazini ni tatizo ambalo linastahili kupatiwa ufumbuzi.

Serikali ya China imetoa wito kwa Marekani kutatua tofauti zao kwa njia ya amani.

Majaribio ya silaha za Nyuklia imeendelea kutishia usalama wa nchi jirani na mataifa jirani kama Japan na Korea Kusini.