MAREKANI-IRAN-USALAMA

Marekani yainyooshea Iran kidole cha lawama

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson aishtumu Iran kufanya uchokozi wa hali ya juu.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson aishtumu Iran kufanya uchokozi wa hali ya juu. REUTERS/Sergei Karpukhin

Serikali ya Marekani kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje Rex Tillerson, imeilaumu Iran kwa kufanya uchokozi wa hali ya juu. Bw Tillerson amesema uchokozi huo unanuia kuvuruga uthabiti katika Mashariki ya Kati na kuhujumu juhudi za Marekani katika ukanda huo.

Matangazo ya kibiashara

Waziti Rex Tillerson amesema Iran inatakiwa ichukuliwe hatua kali isiwezi kwenda njia sawa na ile ya Korea Kaskazini na kushinikiza nchi nyingine kwenye njia hiyo.

Iran mpaka wakati huu haijasema lolote kuhusu madai hayo mapya ya Marekani.

Iran imekanusha mara kadhaa shutuma kutoka kwa nchi za Magharibi kwamba inajaribu kustawisha silaha za nyuklia.

Itafahamika kwamba Rais Donald Trump tayari ameagiza utathmini mpya ufanywe kuhusu mkataba uliotiwa saini kati ya nchi za Magharibi kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran.

Hayo yakijiri vita vya maeneo kati ya Marekani na Korea Kaskazini vimeendelea, huku Marekani ikiituhumu Korea Kaskazini kutoheshimu sheria za kimataifa, na kutishia kuishambulia

Hata hivyo Korea Kaskazini ilionya kwamba itajibu iwapo Marekani itathubutu kuishambulia kijeshi.