MAREKANi-UFILIPINO-USHIRIKIANO

Duterte aalikwa na Trump ikulu ya White House

Rais wa Ufilipino Rodrigo kwenda Washington kwa mwaliko wa rais Donald Trump.
Rais wa Ufilipino Rodrigo kwenda Washington kwa mwaliko wa rais Donald Trump. REUTERS/Erik De Castro

Rais wa Marekani Donald Trump amemualika mwezake wa Ufilipino Rodrigo Duterte kwenda White House baada ya kuwasiliana kwa njia ya simu. Viongozi hawa walifurahia mazungumzo yao.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump na Rodrigo Duterte walishauriana kuhusu vita tata vya Duterte vya kukabiliana na mihadarati, ambavyo vimesababisha kuuawa kwa watu karibu 7,000 katika kipindi cha miezi 12.

Kwa mujibu wa White House, Bw Trump alifurahia sana mazungumzo hayo, na alitoa mwaliko, ingawa tarehe yenyewe ya ziara hiyo haikuafikiwa.

Ziara hiyo itakuwa fursa ya "kujadiliana kuhusu umuhimu wa ushirikiano wa Marekani na Ufilipino, ambao kwa sasa unaendelea kuimarika," taarifa ya White House ilisema.

Mzozo kuhusu Korea Kaskazini pia ulijadiliwa kati ya viongozi hao wawili mjini Washington.

Mwaka uliopita mkutano kati ya Rodrigo Duterte na Barack Obama ulifutwa baada ya Duterte kumuita Obama "mtoto wa kahaba".

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte ameendelea kulaumiwa na jumuiya ya kimataifa kutokana na ukatili wake katika vita dhidi ya madawa ya kulevya nchini Ufilipino.