MAREKANi-USALAMA

Polisi 2 waliomuua Mmarekani mweusi wafutiwa mashtaka Marekani

Alton Sterling, 37 aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 5, 2016, mjini Louisana.
Alton Sterling, 37 aliuawa kwa kupigwa risasi Julai 5, 2016, mjini Louisana. Social Media/Handout via Reuters

Maafisa wawili wa polisi ambao walimuua kwa kumpiga risasi Alton Sterling, Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 37, miezi kumi iliyopita katika eneo la Baton Rouge, mjini Louisiana, na kusababisha maandamano makubwa kote Marekani, wamefutiwa mashtaka yaliyokua yakiwakabili.

Matangazo ya kibiashara

Mwendesha mashtaka Corey Admunson, alisema Jumatano wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika eneo la Baton Rouge kwamba hakuna "ushahidi wa kutosha" ili polisi hao wawili wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Bw Admunson alisema video ya tukio haionyeshi kama Alton Sterling alijaribu kutoa bastola mfukoni mwake, kama ilivyoelezwa na polisi kwa kujitetea kuwa ndio sababu iliyopelekea wanampiga risasi.

Kifo cha Alton Sterling, kiliyonaswa na wapita njia, kilisababisha maandamano na machafuko makali, na kuibua mjadala kuhusu namna watu wachache wanavyoshughulikiwa nchini Marekani.

Wiki mbili baada ya tukio hili, polisi watatu waliuawa katika eneo la Baton Rouge na mshambuliaji ambaye baadaye alijiua kwa risasi.