MAREKANI-OBAMACARE-AFYA

Bunge kupiga kura ya kufutwa kwa huduma ya Obamacare Marekani

Waandamanaji wa Tea Party, Septemba 10, wakipinga mageuzi ya sheri aya huduma ya afya ya nafuu inayojulikana kama Obamacare, mjini Washington.
Waandamanaji wa Tea Party, Septemba 10, wakipinga mageuzi ya sheri aya huduma ya afya ya nafuu inayojulikana kama Obamacare, mjini Washington. REUTERS/Jonathan Ernst

Wabunge wa chama cha Republican wameamua kujaribu tena kwa mara ya pili kupitisha agizo la kufuta na kurejelea sheria ya huduma ya afya ya nafuu inayojulikana kama Obamacare, baada ya kushindwa Machi 24.

Matangazo ya kibiashara

Kevin McCarthy, kiongozi wa wengi bungeni amesema kwamba hatua muhimu imepigwa kuelekea kuidhinishwa mojawapo ya ahadi alizotoa rais Donald Trump wakati wa kampeni.

Kipengele kilichokarabatiwa kinachoahidi dola bilioni 8 kusaidia watu walio na magonjwa ya kitambo, kinaonekana kuwaridhisha waliokuwa na shaka.

Wanachama wa Republican wana imani kwamba sasa wana kura za kutosha.

Jitihada ya awali ya kufutwa kwa sheria hiyo Machi 24 ilishindwa.