VENEZUELA

Wanawake Venezuela waandamana kumpinga raisi Maduro

Wanawake waandamana Caracas,  6 mai 2017.
Wanawake waandamana Caracas, 6 mai 2017. REUTERS/Carlos Garcia Rawlins

Maelfu ya wanawake waliovalia mavazi meupe walifanya maandamano siku ya jumamosi kumshinikiza raisi Nicolas Maduro kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Wakiongozwa na viongozi wa upinzani mawakili na Lilian Tintori mke wa kiongozi wa upinzani aliyefungwa jela Leopoldo Lopez,umati huoulibeba vipeperushi na mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kupinga ukandamizaji.

Awali polisi na wanajeshi walizuia maandamano haya kufika wizara ya mambo ya ndani lakini sasa wanawake hao wameandamana na kuingia wizara ya mambo ya ndani na wizara ya sheria.

Maandamano hayo ni hisia za wakati huu katika kipindi cha zaidi ya mwezi wa maandamano dhidi ya serikali ambapo mengi yalikuwa yakikabiliana na wafuasi wa raisi Maduro na vikosi vya usalama.

Idadi ya watu waliopoteza maisha tangu mwezi April maandamano yalipoanza wakati raisi Maduro na serikali yake ikifanya jitihada za kukandamiza upinzani ni walau watu 36 kwa mujibu wa mwendesha mashtaka huku majeruhi wakizidi mia moja.