MAREKANi-TRUMP-COMEY-HAKI

Donald Trump: Comey alipoteza imani katika kila mtu Washington

Donald Trump amesema hatua ya kumfuta kazi James Comey inaeleweka.
Donald Trump amesema hatua ya kumfuta kazi James Comey inaeleweka. REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump amesema karibuni wabunge wa vyama vya Democratic na Republican watamshukuru kwa kumfuta kazi mkuu wa FBI James Comey. Wengi wameeleza kushangaa kwao kwa uamuzi huo, ikizingatiwa kwamba Bw Trump mwenyewe alimsifu kwa jinsi alivyofuatilia na kuongoza uchunguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

Bw Comey alikuwa anaongoza uchunguzi wa FBI kuhusu uhusiano kati ya maafisa wa kampeni wa Trump na Urusi.

Donald Trump alimfuta kazi kutokana na jinsi alivyoshughulikia uchunguzi wa barua pepe za Hillary Clinton, aliye pambana na rais Donald Trump katika uchaguzi wa Marekani mwaka jana.

Rais Donald Trump ametetea uamuzi wake ulioshangaza wengi wa kumfuta kazi mkuu huyo wa Shirika la Ujasusi nchini Marekani (FBI), akisem akuwa hatua yake itawafurahisha wengi katika siku za usoni.

Kufutwa kwake "kuzua maswali kuhusu iwapo ikulu ya White House inaingilia wazi uchunguzi wa jinai," alisema Adam Schiff.

Adam Schiff ni mwanachama wa ngazi ya juu zaidi kutoka chama cha Democratic katika kamati ya bunge kuhusu ujasusi.

Lakini kiongozi huyo ametetea uamuzi wake Jumatano asubuhi, saa chache kabla ya kukutana na waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov, mkutano wa kwanza kati ya Trump na maafisa wa Urusi tangu achukue hatamu Januari.

Hii ni mara ya pili pekee kwa mkuu wa FBI kufutwa kazi katika historia ya Marekani.