MAREKANI-UDUKUZI

Mataifa mia moja yaathirika na mashambulizi ya kimtandao

Mashambulizi ya kimtandao yaathiri mataifa mia moja duniani
Mashambulizi ya kimtandao yaathiri mataifa mia moja duniani Pixabay

Mashambulizi ya kimtandao kwa kutumia vifaa vya udukuzi vinavyoaminika kutengenezwa na idara ya usalama wa taifa la Marekani NSA yameathiri maelfu ya kompyuta za takribani mataifa mia moja.

Matangazo ya kibiashara

Watafiti wenye mbinu za kiusalama za kukabiliana na athari hizo wamethibitisha athari zaidi ya elfu hamsini kwa mataifa 99 ikiwemo Urusi Ukraine na Taiwan mlengwa nambari moja.

Wizara ya mambo ya ndani nchini Urusi imesema baadhi ya kompyuta zake zimeshambuliwa na virusi.

Msemaji wa wizara hiyo Irina Volk ameliambia shirika la habari la Urusi kuwa imerekodi mashambulizi ya kimtandao katika kompyuta za wizara zinazoendeshwa kwa mfumo wa Window.

Hata hivyo amedai hatua zimechukuliwa kwa lengo la kuangamiza na kudhibiti virusi hivyo.