MAREKANi-URUSI-VYOMBO VYA HABARI

Vyombo vya habari Marekani vyamuweka Trump matatani

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Donald Trump alimtaka James Comey kusitisha uchunguzi wake dhidi ya General Flynn.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Donald Trump alimtaka James Comey kusitisha uchunguzi wake dhidi ya General Flynn. REUTERS/Kevin Lamarque

Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kukumbwa na kasha mbalimbali. Baada ya jarida la Washington Post kufichua taarifa za siri zilizowasilishwa kwa Urusi, kufuatia kesi ya Jenerali Michael Flyn, inaaminiwa kuwa rais Trump aliingilia kazi ya shirika la ujasusi la Marekani la FBI.

Matangazo ya kibiashara

Magazeti kadhaa nchini Marekani yanadai kuwa rais Donald Trump aliomba mkurugenzi wa FBI kusitisha uchunguzi kuhusu Jenerali Flynn. Kesi hii sasa imechukuliwa kwa umakini mkubwa na wawakilishi wa Bunge la Congress.

Kwa mujibu wa The New York Times, moja ya magazeti hayo, rais Donald Trump alimtaka aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la FBI James Comey kusitisha uchunguzi uliokuwa ukiendelea dhidi ya aliyekuwa mshauri wa maswala ya usalama Michael Flynn.

Ikulu ya Whitehouse imekana ripoti hiyo katika taarifa, ikisema kwamba rais Trump hajamtaka James Comey ama mtu yeyote kusitisha uchunguzi ikiwemo uchunguzi wowote unaohusiana na jenerali Michael Flynn.

Kwa mujibu wa barua ilioandikwa na james Comey, rais Donald Trump aliniambia baada ya mkutano katika Ikulu ya White House mnamo mwezi Februari, “nadhami ni vizuri uachane na uchunguzi huo.”

Vyombo vya habari vya Marekani vinabaini kwamba barua hiyo iliandikwa mara moja baada ya mkutano, siku moja baada ya Michael Flynn kujiuzulu.

Bwana Flynn alijiuzulu mnamo mwezi Februari baada ya kumdanganya Makamu wa Rais kuhusu mazungumzo yake na balozi wa Urusi kabla ya Trump kuchukua mamlaka.