BRAZIL-UFISADI

Rais Michel Temer ashinikizwa kujiuzulu kwa madai ya ufisadi

Rais wa Brazil Michel Temer
Rais wa Brazil Michel Temer REUTERS/Ueslei Marcelino/File Photo

Wanasiasa wa upinzani na waandamanaji nchini Brazil wanashinikiza kujiuzulu kwa rais Michel Temer.

Matangazo ya kibiashara

Hii imekuja baada ya kubainika kuwa alinaswa katika mazungumzo ya siri akijadili malipo kutoka kwa mshukiwa wa ufisadi, ili asiwe shahidi katika kesi inayomkabili.

Ripoti zinasema kuwa tayari mazungumzo hayo yamewasilishwa kwa viongozi wa Mashtaka nchini humo kwa mujibu wa Gazeti la O Globo lililoandika ripoti hiyo.

Inaripotiwa kuwa rais Temer, aliagiza kuwa shahidi huyo Eduardo Cunha, ambaye ni Spika wa zamani na anayeshikiliwa, alipokea Mamilioni ya Dolla kutaka kashfa ya ufisadi kutoka shiriika la mafuta la serikali la Petrobras.

Hata hivyo, Ofisi yake imekanusha kuwa rais Temer alihusika katika mazungumzo yoyote ya kupokea fedha kama ilivyoripotiwa.

Kabla ya kuzuiwa, Cunha ambaye alikuwa ni mshirika wa karibu wa chama cha rais Temer, alikuwa na taarifa muhimu kuhusu wanasiasa wakubwa nchini humo wanaohusika na wizi wa fedha katika shirika hilo la mafuta.