MAREKANI-URUSI-TRUMP-HAKI

Robert Mueller kuchunguza tuhuma kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani

Robert Mueller, aliekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la FBI kuanzia 2001 hadi 2013.
Robert Mueller, aliekuwa mkuu wa shirika la ujasusi la FBI kuanzia 2001 hadi 2013. REUTERS/Yuri Gripas

Wizara ya sheria nchini Marekani, imetangaza kwamba aliekua kiongozi wa zamani wa shirika la kijasusi la FBI, Robert Mueller, ameteuliwa kuwa mwendesha mashtaka maalum atakae ongoza uchuguzi wa tuhuma kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani wa mwaka uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Pia katika uchunguzi wake, Robert Mueller atazingatia iwapo kulikuwa na mwingiliano wa aina yoyote kati ya Urusi na timu ya kampeni ya Trump.

Tangazo hilo linafuatia utata ulioibuka kufuatia kufutwa kazi kwa James Comey wiki moja iliyopita. James Comey ndie alikuwa akiongoza uchunguzi huo.

Taarifa iliyotolewa na wizara ya sheria nchini Marekani imebaini kwamba uchunguzi huo utaongozwa na mtu asiyeegemea upande wowote kwa ajili ya maslahi ya umma.

Itafahamika kwamba Robert Mueller aliwahi kuwa mkuu wa shirika la kijajusi la FBI kuanzia 2001 - 2013 .