Trump kuwahotubia viongozi wa nchi za kiarabu kuhusu ugaidi
Imechapishwa: Imehaririwa:
Rais wa Marekani Donald Trump anakutana na viongozi wa nchi za kiarabu na wakuu wa dini ya Kislamu nchini Saudi Arabia.
Trump ambaye amefanya ziara yake ya kwanza nje ya nchu tangu kuingia madarakani mwezi Januari, anatarajiwa kuwaambia viongozi wa nchi hizo kuunganisha nguvu kupambana na ugaidi na itikadi kali.
Kiongozi huyo wa Marekani anatarajiwa pia kueleza mpango wa serikali yake kupambana na ugaidi hasa kundi la Islamic State ambalo limeendelea kuwa tishio kwa mataifa mabalimbali ya kiarabu.
Katika ziara yake ya kwanza siku ya Jumamosi, Trump alitia saini mkataba wa kibiashara unaokadiriwa kuwa zaidi ya Dola 350 na serikali ya Saudi Arabia na pia kukubaliana kushirikiana katika maswala ya kiusalama.
Ni ziara inayokuja miezi miwili baada ya Trump kutangaza kuzuia raia kutoka nchi tisa za Kiislamu kwenda Marekani, uamuzi ambao hata hivyo ulizuiwa na Mahakama.
Baada ya kuondoka nchini Saudi Arabia, Trump amesema hivi karibuni atatembelea nchi ya Misri.