VENEZUELA-MAANDAMANO-USALAMA

Madaktari waandamana dhidi ya rais Maduro nchini Veneuela

Madaktari na wafanyakazi wa afya waandamana Mei 22, 2017 katika mji wa  Caracas.
Madaktari na wafanyakazi wa afya waandamana Mei 22, 2017 katika mji wa Caracas. AFP

Madaktari na wafanyakazi wa afya waliandamana Jumatatu hii Mei 22, 2017 katika mji wa Caracas, chini Venezuela. Hata hivyo Rais Nicolas Maduro ameitisha msafara wa amani siku ya Jumanne. 

Matangazo ya kibiashara

Maandamano ya Madaktari ya Jumatatu katika mji wa Caracas yaliingia katika kuashiria wiki ya nane ya uhamasishaji dhidi ya rais wa Venezuela Nicolas Maduro, maandamano ambayo yamesababisha mpaka sasa vifo vya watu vifo vya watu 48.

Kambi zote mbili zinajipima nguvu kwa mara nyingine, ikiwa ni pamoja na gwaride la shirikisho la wafanyakazi nchini Venezuela (FMV) ambao waliandamana kuelekea makao makuu ya wizara ya Afya, huku wakiungwa mkono na upinzani, kabla ya msafara wa amani ulioitishwa siku ya Jumanne na rais Nicolas Maduro.

"Lazima kuongeza shinikizo kulingana na hali inavyokwenda," alisema kiongozi wa upinzani Henrique Capriles.

Siku ya Jumatatu asubuhi, makabiliano yalishuhudiwa kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nje kidogo ya mji mkuu wa nchi hiyo na vizuizi vilikua viliwekwa kwenye barabara nyingi.

"Wanawazuia madaktari kutoka manispaa yetu kushiriki katika maandamano", David Smolansky, Meya wa wilaya ya El Hatillo, katika mashariki ya mji. Bw El Hatillo ni kutoka upinzani

Pamoja na makabiliano na mabomu ya machozi, wapinzani wa rais Nicolas Maduro wameendelea kuwa imara, wakichukizwa na kuanguka kwa uchumi wa nchi yao.