MAREKANI-VATICAN-USHIRIKIANO

Papa Francis na Donald Trump wazungumzia kuhusu amani

Papa Francis na Donald Trump Mei 24 mjini Vatican.
Papa Francis na Donald Trump Mei 24 mjini Vatican. REUTERS/Alessandra Tarantino

Rais wa Marekani Donald Trump amepokelewa Jumatano hii na mwenyeji wake Papa Francis, kiongozi wa kanisa Katoliki. Rais wa Marekani alikutana kwa mara ya kwanza Mei 24, 2017 na kiongozi wa Kanisa katoliki duniani, fursa ya kujadili mada nyeti wanazotofautiana.

Matangazo ya kibiashara

Mkutano iliyoanza katika hali ya wasiwasi, lakini uliendelea vizuri baadaye. Papa alimtaka rais wa Marekani kuwa"chombo cha amani" duniani.

Papa Francis alimpokea rais wa Marekani, kama kwamba alikuwa na haraka ya kukutana na mwenyeji wake. Mazungumzo yao yalidumu nusu saa. Katika ajenda ya mazungumzo yao, Trump alitaka kusikia kama ahadi ya uhuru wa dini na dhamira, lakini makao makuu ya Vatican yalisema majadiliano yalilenga ahadi ya kanisa Katoliki la Marekani katika sekta ya afya, elimu na msaada kwa wahamiaji, mada nyeti nchini Marekani.

"Chombo cha amani"

Mazungumzo kuhusu amani ndio yalitawala mkutano wa viongozi hao wawili. Kama ishara, Papa Francis amempa Trump ujumbe wake kwa siku ya Amani Duniani, ambayo yeye binafsi alisaini, "ninakupa ujumbe huu ili uwe chombo cha amani," alisema Papa kwa Rais wa Marekani aliwasili Vatican akitokea nchini Saudi Arabia baada ya kusaini mkataba wa mauzo ya silaha. Mkataba ambao ulipokelewa vibaya na Vatican. "Tunahitaji amani," Donald Trump alijibu.

"Papa ni kiongozi mkuu"

Mkutano ulimalizika katika hali nzuri. "Sintosahau ulichosema," alisema Donald Trump akimsabahi Papa Francis, kabla ya kwenda kukutana na Katibu Dola wa Makao makuu ya Vatican, Kardinali Parolin. "Tulikuwa na mazungumzo mazuri, alisema rais wa Marekani, saa chache baada ya mkutano, Papa ni kiongozi mkuu, " ameomngeza rais Trump.

Rais Donald Trump akimsabahi Papa Francis, Mei 24, 2017.
Rais Donald Trump akimsabahi Papa Francis, Mei 24, 2017. REUTERS/Alessandra Tarantino/Pool