Askari wasambazwa Brasilia kudhibiti hali ya mambo
Imechapishwa:
Rais wa Brazil Michel Temer ametuma majeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Brasilia, baada ya waandamanaji kuanza kulichoma moto jengo la serikali na kuharibu mengine.
Kuna wasiwasi kwamba kusambazwa kwa wanajeshi kudhibiti mambo kunaweza kuchochea zaidi vurugu.
Tuhuma za rushwa zinazomkabili rais wa nchi hiyo ndizo zilizosababisha mchafuko hhayo ya kisiasa.
Maafisa wanasema hatua hiyo ni muhimu kwa ajili ya kudhibiti hali ya usalama, baada ya waandamanaji elfu 35 waliokuwa wakielekea mjini na kuongoza moja kwa moja katika bunge la nchi hiyo na katika makazi ya rais.
Polisi wamefyatua mabomu ya machozi katika umati wa watu. Walipokua wakijaribu kuwatawanya waandamanaji.
Maandamano yamekua yakiendelea katika mji mbalimbali nchini Brazil, ambapo waandamanaji wanadai rais wa nchi hiyo ajiuzulu kutokana na kashfa za rushwa zinazomkabili.