MAREKANI-FBI-UCHUNGUZI

Mkwe wa Trump, Jared Kushner, achunguzwa na FBI

Jared Kushnerna mkewe Ivanka Trump, Machi 17, 2017.
Jared Kushnerna mkewe Ivanka Trump, Machi 17, 2017. REUTERS/Jim Bourg

Shirika la ujasusi la FBI linamchunguza mkwe wa rais Donald Trump na mshauri mkuu Jared Kushner ikiwa ni miongoni mwa kesi ya uchunguzi wa Urusi kulingana na vyombo vya habari nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

FBI inachunguza hatua ya Urusi kuingilia uchaguzi wa urais wa 2016 nchini humo na ushirikiano wa kundi la kampeni la rais Trump.

Wakili wa bwana Kushner amesema kuwa mteja wake atashirikiana na wachunguzi hao kuhusu uchunguzi wowote.

Ripoti zinasema kuwa wachunguzi wanaamini ana habari muhimu lakini sio mshukiwa wa uhalifu.
Rais Trump mefutilia mbali madai yoyote ya kujihusisha na Urusi wakati wa kampeni.

Gazeti la Washington Post limeripoti kwamba wachunguzi hao walikuwa wakiangazia mikutano aliofanya mwaka uliopita na balozi wa Urusi nchini Marekani ,Sergei Kislyak na mfanyikazi mmoja wa benki kutoka Moscow.

Vitengo vya ujasusi vinaamini Moscow ilijaribu kukisaidia chama cha Republican kushinda uchaguzi huo dhidi ya Hillary Clinton, mgombea wa chama cha Democrat.