BRAZIL-USALAMA-HAKI

Rais wa Brazil asitisha mpango wake wa kutuma jeshi Brasilia

Rais wa Brazil Michel Temer, hapa katika ikulu ya rais rmjini Brasilia, Mei 20, 2017.
Rais wa Brazil Michel Temer, hapa katika ikulu ya rais rmjini Brasilia, Mei 20, 2017. REUTERS/Ueslei Marcelino

Nchini Brazil, rais wa Michel Temer amechukua uamuzi wa kuachana na mpango wake wa kusambaza jeshi katika mji mkuu wa nchi hiyo Brasialia katika hali ya kukabiliana na waandamanaji wanaoendelea kuandamana.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, Mei 24, askari 1500 walitumwa katika mji wa Brasilia kulinda majengo ya serikali baada ya waandamanaji wanaomtaka rais Temer kujiuzulu kuchoma baadhi ya majengo ya serikali. Rais Temer anatuhumia ufisadi. Rais Michel Temer alifuta amri hiyo kwa muda usiozidi masaa 24 baada ya kusaini. Lakini bado anaendelea kutishiwa.

"Machafuko hayavumiliwa, " amesema Waziri wa Ulinzi ambaye alikutangaza kuondolewa kwa jeshi katika mji mkuu. Muda mfupi kabla, rais Temer aliuta amri inayoidhinisha kupelekwa kwa jeshi katika mji mkuu baada ya makabiliano makali wakati wa maandamano yalitoendeshwa nje jengo la Bunge. Katika makabiliano watu zaidi ya arobani walijeruhiwa, lakini pia majengo mbalimbali ya serikali yalichomwa moto.

Wakati huo huo hali ya utlivu ilirejea katika mji wa Brasilia, lakini amri ya rais Temer ilikosolewa kwa kutolea wito jeshi kukabiliana vikali na waandamanaji katika mji huo. Hata rais Temer alifuta amri hiyo.

Muda mfupi baadaye, Chama cha mawakili kiliomba bunge kumtimu rais Temer. bunge la taifa linamuunga mkono rais Michel Temer anaelengwa na Mahakama kuu kwa kashfa ya ufisadi na kushiriki katika kundi la wahalifu." anahusishwa katika kashfa mbaya ya rushwa katika historia ya nchi hiyo inayo sekta zote za kisiasa nchini Brazil.