MAREKANI-URUSI-USALAMA

Bunge la Marekani: Wakili wa Trump atakiwa kuchunguzwa

washirik awa karibu wa rais wa Marekani Donald Trump waendelea kukabiliwa na tuhuma mbalimbali, hasa tuhuma kuhusu muingilio wa Urusi katika masuala ya usalama wa Marekani.
washirik awa karibu wa rais wa Marekani Donald Trump waendelea kukabiliwa na tuhuma mbalimbali, hasa tuhuma kuhusu muingilio wa Urusi katika masuala ya usalama wa Marekani. REUTERS/Jonathan Ernst

Jopo la Bunge nchini Marekani limeomba wakili wa rais Donald Trump, Michael Cohen, achunguzwe kuhusu muingiio wa Urusi katika uchaguzi wa Marekani. Wiki iliopita mkwe wa rais Trump, Jared Kushner, alitajwa katika uchunguzi huo wa Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Michael Cohen alisema kuwa alikataa ombi hilo kwa kuwa liliangazia maswala mengi ambayo alujikuta ni vigumu kwake kujibu.
Michael Cohen ameviambia vyombo vya habari vya Marekani kwamba alitakiwa kutoa habari na ushahidi kuhusu mawasiliano aliyokuwa nayo na ikulu ya rais wa Urusi.

“Nilikataa mwaliko huo kushiriki kwa kuwa wito wenyewe ulikuwa umeangaziwa vibaya, ukigusia maswala mengi ambayo sina uwezo kujibu”, Bw Cohen ameviambia vyombo vya habari.

Itafahamika kwamba Michael Cohen ni mshirika wa karibu wa Trump ambaye amekukataa kuhusishwa na uchunguzi huo.