MAREKANI-USALAMA

Marekani yafanikiwa mfumo wa kutegua makombora

Kombora ICBM lilisafiri kwa urefu wa kilomita 450 kabla ya kuanguka katika maji ya Japan.
Kombora ICBM lilisafiri kwa urefu wa kilomita 450 kabla ya kuanguka katika maji ya Japan. U.S. Department of Defense, Missile Defense Agency/Handout via R

Marekani imeujaribu mfumo wake wa kutegua makombora ya masafa marefu ICBM. Mfumo huo ulirushwa kutoka Kwa Jalein Atoll katika kisiwa cha Marshal juu ya anga ya Pacific,

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama, Marekani kwa mara ya kwanza imefanikiwa kuufanya majaribio mfumo wake wa kudungua makombora ya masafa marefu.
Pentagon imesema kuwa majaribio hayo yalikuwa yamepangwa muda mrefu uliopita, kwa wakati huu mfumo huo umefanikiwa wakati ambapo wasiwasi mkubwa na Korea Kaskazini bado unaendelea.

Tangazo hilo linajiri baada ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio kombora lake la tatu katika kipindi cha wiki tatu.

Kombora hilo lilisafiri kwa urefu wa kilomita 450 kabla ya kuanguka katika maji ya Japan.

Mfumo huo wa ardhini uliwekwa katika kambi moja ya kijeshi mjini California na kudungua kombora la masafa marefu kulingana na kitengo cha ulinzi wa makombora MDA.