MAREKANI-HALI YA HEWA-TRUMP

Trump kutangaza uamuzi wake Alhamisi hii kuhusu mkataba wa Paris

Donald Trump, Washington, tarehe 17 Mei.
Donald Trump, Washington, tarehe 17 Mei. REUTERS/Yuri Gripas

Rais wa Marekani Donald Trump anatazamiwa kutangaza uamuzi wake leo Alhamisi kuhusu mkataba wa mabadiliko hali ya hewa ulioafikiwa mjini Paris, nchini Ufaransa. Kuondoka kwa Marekani itakuwa ni pigo kubwa, miezi kumi na nane baada ya mkataba huu wa kihistoria kuafikiwa, ambapo Beijing na Washington, chini ya usimamizi wa rais Barack Obama.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump atatoa uamuzi wake Alhamisi hii mchana kuhusu Marekani kutoka au la kwenye mkataba wa Paris katika kupambana na ongezeko la joto duniani. rais donald Trump alitangaza kwenye Twitter Jumatano usiku.

Ulimwengu mzima uliku ukisubiri uamuzi huo. Tangu siku ya Jumatano mchana, vyombo vya habari kadhaa vya Marekani vilitangaza nia ya rais wa Marekani kujiondoa kwenye mkataba huo ulifikiwa mwishoni mwa mwaka 2015 katika mji mkuu wa Ufaransa na nchi zaidi ya 190 chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa. Mkataba huu unalenga kupunguza kuongezeka kwa joto duniani kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu.

"Nitatangaza uamuzi wangu kwenye mkataba wa Paris katika siku zijazo," Donald Trump alionya siku ya Jumatano usiku. Tangu kuingia madarakani, Donald trump ameendelea kuonyesha nia yake ya kuongeza nishati mbadala (makaa ya mawe, mafuta, gesi), kwa niaba ya ulinzi wa ajira Marekani. Wakati wa kampeni zake, Donald Trump ambaye alieleza kwamba anataka kukomesha "vita dhidi ya makaa ya mawe," aliahidi "kufuta" mkataba huo. Pamoja na kuchukua hatamu ya uongozi tarehe 20 Januari, alituma ishara zilizotafautiana, kuhusu nishati kwa njia tatanisha kwa serikali yake juu ya suala la hali ya hewa, lakini pia zaidi, jukumu la Marekani duniani na uhusiano wake kwaushirikiano wa kimataifa.

Suala kupambana na ongezeko la joto duniani liliwagawanya viongozi walioshiriki mkutano wa nchi saba zilizostawi kiuchumi (G7) uliofanyika hivi karibuni katika mji wa Sicily nchini Italia, ambapo washiriki wote isipokuwa Donald Trump, walionyesha ahadi zao kwa mkataba huo.