MAREKANI-ORLANDO-USALAMA

Watu zaidi ya 49 waangamia katika shambulizi Orlando

Polisi katika jimbo la Florida inasema kuwa watu kadhaa wameuwawa baada ya kushambuliwa kwa risasi katika eneo la viwandani mjini Orlando, nchini Marekani.

Mtoto akicheza kando ya misalaba 49 ya mbao iliowekwa kwenye makabui ya Orlando kwa waathirika wa mashambulizi ya Pulse.
Mtoto akicheza kando ya misalaba 49 ya mbao iliowekwa kwenye makabui ya Orlando kwa waathirika wa mashambulizi ya Pulse. REUTERS/Carlo Allegri
Matangazo ya kibiashara

Tukio hili ambalo linatokea wiki moja kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza ya shambulio katika klabu moja ya usiku ya Pulse mjini humo, ambapo watu 49 waliuwawa, lilitokea mapema Jumatatu asubuhi, mashariki mwa mji huo, gazeti la Orlando Sentinel, limearifu.

Afisa mkuu wa polisi katika kaunti ya Orange, anatarajiwa kutoa taarifa kwa waandishi habari muda mchache ujao.

Awali polisi waliasema walizingira eneo la tukio.

Maafisa wa usalama katika jimbo la Florida wanasema kuwa mauwaji hayo yalitokea katika eneo moja la biashara ya kuunda hema na vifaa vya kupiga kambi.

Itafahamika kwamba mwaka jana, Omar Mateen, aliwaua kwa risasi watu 49 na kuwajeruhi wengine wengi katika klabu moja ya usiku ya wapenzi wa jinsia moja, kabla ya kuuliwa na polisi.