MAREKANI-URUSI-USALAMA

Mkuu wa zamani wa FBI athibitisha kushinikizwa na Trump

Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) na aliyekuwa Mkurugenziwa FBI James Comey (kulia).
Rais wa Marekani Donald Trump (kushoto) na aliyekuwa Mkurugenziwa FBI James Comey (kulia). REUTERS/Jim Lo Scalzo/Pool, Gary Cameron/File Photo

Mkurugenzi wa zamani wa shirika la ujasusi la FBI, James Comey anatazamia kutoa ushahidi Alhamisi hii, Juni 8, 2017 mbele ya bunge la Congress kuhusu uwezekano wa Urusi kuingilia katika kampeni za uchaguzi wa Marekani, na uhusiano wa timu ya Trump na Urusi.

Matangazo ya kibiashara

Bunge la Seneti lilichapisha taarifa ya awali ya James Comey. Taarifa hii inathibitisha majaribio ya rais Donald Trump ya kumshawishi aliyekuwa mkurugenzi wa FBI.

James Comey amewaambia wabunge wa Congress kuwa kabla ya kufutwa kwaka kazi, rais Donald Trump alimshinikiza kumtii katika kila jambo.

Aidha, Comey amesema rais Trump alimtaka kuachana na uchunguzi wa ni kwanini alimfuta kazi mshauri wake wa maswala ya usalama Mike Flynn.

Ameongeza kuwa alimwambia Trump kuwa hamchunguzi kuhusu madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani huku Trump kupitia Mawakili wake akisema kuwa ameridhishwa na kauli hiyo ya Comey.

Bw Comey amesema rais Trump alimtaka kuacha kumchunguza mshauri wa zamani wa masuala ya usalama ambaye alijiuzulu kufutia shutma kuwa alikua akibadilishana habari na urusi na hivyo kushutumiwa kuhatarisha usalama wa ndani wa Marekani.

Wakili wa Trump amesema rais Trump anahisi kuna ukweli kwa uthibitisho kuwa yeye mwenyewe binafsi hakuwa akichunguzwa kwa timu yake ya kampeni zake kuhusishwa na Urusi.

Maafisa wawili wanaohusika na usalama, Mike Rogers na Dan Coats wamewaambia maseneta kuwa hawakuwahi kulazimishwa kufanya jambo lolote ambalo liko kinyume na sheria.

James Comey alitoa ushahidi wa mazungumzo kati yake na rais Donald Trump aliyofanya naye mara tano wakati Trump alipokuwa akirudia kutaka amsikilize.

James Comey anasema alikuwa akifanya kazi zake bila kuegemea upande wowote na alimuheshimu sana rais Trump na hakutaka kuonyesha kuwa alidharau yale aliomtaka kufanya.