MAREKANI

Rais Trump afutilia mbali madai ya Comey

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Jonathan Ernst/File Photo

Rais Trump afutilia mbali tuhuma za aliyekuwa Mkuu wa Shirika la Ujasusi Comey kuhusu madai aliyatoa katika mbele ya Kamati ya Inteljensia ya Senate siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Trump kupitia wake wake binafsi Marc Kaswitz, kiongozi huyo amesema Comey ndiye anayestahili kuchunguzwa kuhusu yale aliyoyasema.

Mkuu huyo wa zamani wa FBI aliwaambia Maseneta hao kuwa rais Trump aliwambia kuwa ni alitarajia kuwa atamtii lakini pia alimwagiza kuacha kumchunguza Michael Flynn, aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama.

Aidha, aliwaambia Maseneta hao kuwa alikuwa na uhakika kuwa Urusi iliingia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2016.

Urusi hata hivyo, umekanusha madai hayo.

Rais Trump alimfuta kazi Comey kwa madai kuwa Shirika la FBI lilikuwa limekosa imani naye, madai ambayo amekuwa akikanusha.