DONALD TRUMP-MAREKANI

Trump apata pigo tena, mahakama yapinga amri yake ya kuzuia wageni

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. ©REUTERS/Jonathan Ernst

Mahakama ya rufaa nchini Marekani imezuia kwa mara nyingine kutekelezwa kwa amri ya rais Donald Trump kuhusu makataa ya kuingia nchini humo kwa wageni kutoka kwenye mataifa 6 ya kiislamu, uamuzi ambao umeendelea kuwa pigo kwa utawala wake.

Matangazo ya kibiashara

Mahakama ya rufaa kwenye jimbo la Circuit imekataa kufuta hukumu ya awali iliyotolewa kwenye mahakama kuu ikizuia kutekelezwa kwa amri ya rais Trump, ikisema kiongozi huyo alivuka mipaka ya madaraka yake kwa kutoa makataa ya kibaguzi.

Hata hivyo shauri hili limepelekwa kwenye mahakama ya juu ya nchi hiyo baada ya mahakama nyingine kutoa uamuzi kinyume na matarajio na wabunge kadhaa wa chama cha Republican ambapo wizara ya sheria imetaka mahakama kuu kusikiliza tena shauri hilo.

Uamuzi wa mahakama ya Circuit umechukuliwa kama pigo jingine kwa utawala wa rais Trump aliyepania kuhakikisha makataa yake ya kuingia nchini humo kwa raia wa kiislamu kutoka kwenye nchin 6 za kiislamu inatekelezwa.

Majaji wa tatu waliosikiliza kesi hiyo na ambao waliteuliwa wakati wa utawala wa rais Bill Clinton wote kwa pamoja waliunga mkono uamuzi uliotolewa kwenye mahakama kuu, kuzuia makataa ya rais Trump wakisema alivuka mipaka ya madaraka yake kisheria.