MAREKANI-KOREA KASKAZINI-VIKWAZO

Marekani kuweka vikwazo dhidi ya washirika wa Korea Kaskazini

Rex Tillerson amesisitiza kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo.
Rex Tillerson amesisitiza kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo. REUTERS/Kevin Lamarque

Serikali ya Marekani kupitia Waziri wa mambo ya Nje Rex Tillerson, imetangaza kwamba itawawekea vikwazo washirika wa kibiashara wa Korea Kaskazini. Marekani imeendelea kuionya Korea Kaskazini kufuatia mpango wake wa kurusha makombora ya masafa marefu.

Matangazo ya kibiashara

Marekani imeamua kuiwekea shinikizo zaidi Korea Kaskazini kutokana na mpango wake wa nuklia na kuendelea kurusha makombora ya masafa marefu na kuishtumu nchi hiyo kuhatarish ausalama wa dunia.

Rex Tillerson amesisitiza kuwa Ikulu ya White House hivi karibuni itaamua ikiwa itaziwekea vikwazo nchi hizo.

Rex Tillerson alitoa onyo hili wakati wa kikao cha bunge kuhusu mahusiano ya ya kigeni siku ya Jumanne Juni 13.

Inasemekana kuwa Korea Kaskazini imepiga hatua katika kuunda makombora ya masafa marefu yenye uwezo wa kufika nchini Marekani.

Umoja wa Mataifa umeendelea kuishtumu Korea Kaskazini kufuatia majaribio yake ya makombora ya hivi karibuni.