MAREKANI-USALAMA

Mfuasi wa Sanders ashambulia kwa risasi wafuasi wa Chama cha Republican

Eneo la usalama latengwa mara moja kwenye eneo la tukio, katika mji wa Alexandria, karibu na mji wa Washington, Juni 14, 2017.
Eneo la usalama latengwa mara moja kwenye eneo la tukio, katika mji wa Alexandria, karibu na mji wa Washington, Juni 14, 2017. REUTERS/Joshua Roberts

Steve Scalise, mmoja wa viongozi wa Chama cha Republican, alijeruhiwa"vibaya" siku ya Jumatano wakati wa shambulio kwenye uwanja wa michezo unaotembelewa mara kwa mara na wabunge wa Congress.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo la risasi lilitokea katika mji wa Alexandria, katika jimbo la Virginia, karibu na mji wa Washington. Shambulizi hili liliwajeruhi watu watano.

Gavana wa jimbo la Virginia, ambae ni kutoka chama cha Democratic, haraka alitembelea eneo la tukio. Terry McAuliffe alisema kuwa kila siku watu 93 wanauawa nchini Marekani 93 na zaidi ya 200 kujeruhiwa kwa bunduki, "Tuna silaha nyingi sana ambazo ziko mikononi mwa raia. Huu si mjadala kwa sasa, lakini ninasema kila siku kwa sababu ni tatizo kubwa sana. "

Mshambuliaji ambaye alifariki kwa majeraha, inaaminiwa kuwa ni mmfuasi kutoka mrengo wa kushoto, mwenye umri wa miaka 66, ambaye alionyesha kumuunga mkono Bernie Sanders, mgombea alieshindwa katika kura za mchujo za uchaguzi wa urais nchini Marekani.

Mnamo mwezi Machi aliandika kwenye ukurasa wake wa Face Book: "Trump ni msaliti. Trump ameharibu demokrasia yetu. Wakati umefika wa kumfuta Trump na watu wake."