MAREKANI-DONALD TRUMP

Rais Trump achunguzwa kwa tuhma za kujaribu kuzuia haki

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump ©REUTERS/Jonathan Ernst

Vyombo vya Habari nchini Marekani vinaripoti kuwa rais Donald Trump anachunguzwa na wakili maalum Robert Mueller kwa tuhma za kuzuia haki.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa juu wa Inteljensia nchini humo wanatarajiwa kuhojiwa kufahamu ukweli uliomfanya rais Trump kuagiza kusitishwa kwa uchunguzi wa aliyekuwa mshauri wake wa maswala ya usalama Michael Flynn.

Washauri wa rais Trump wamesema wameshangazwa sana na kuvuja kwa kinachoendelea kwa vyombo vya Habari.

Ripoti ya uchunguzi huu imechapishwa katika magazeti ya Washington Post, New York Times na Wall Street Journal.

Kazi kubwa ya Mueller ni kubaini ikiwa kuna ukweli kuwa Urusi uliingia uchaguzi Mkuu mwezi uliopita, uliompa ushindi Donald Trump.

Hivi karibuni aliyekuwa Mkuu shirika la ujasusi la FBI James Comey alidai kuwa uwezekano mkubwa wa Urusi kuingilia uchaguzi huo.

Madai haya yamekanushwa na Urusi.

Wiki iliyopita, Kamati ya Senate inayoshughulikia maswala ya Inteljensia ilimhoji Comey na kuibua madai hayo ambayo pia Trump ameyakanusha vikali.