MAREKANI-TRUMP-USALAMA

Donald Trump: Sijawahi kurekodi mazungmzo ya siri na James Comey

Ushahidi tu ya mazungumzo ya siri kati ya Donald Trump na James Comey unatakiwa kuwa mikononi mwa wachunguzi.
Ushahidi tu ya mazungumzo ya siri kati ya Donald Trump na James Comey unatakiwa kuwa mikononi mwa wachunguzi. REUTERS/Mike Theiler

Rais wa Marekani Donald Trump amesema hakuwahi kurekodi mazungumzo ya siri na aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la upepelezi FBI James Comey.

Matangazo ya kibiashara

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump amesisistiza kuwa hana rekodi hiyo siku moja moja kabla ya kuombwa na Congress kuiwasilisha ili kufanikisha uchunguzi wao.

Hata hivyo, hapo awali Trump aliwahi kunukuliwa akisema kuwa alikuwa na hifadhi ya mazungumzo yake na Comey, baada ya kumfuta kazi.

Rais wa Marekani alipewa muda hadi Ijumaa hii awe amekabidhi rekodi hizo kwa Bunge la Congress, wakati ambapo uchunguzi kuhusu Urusi ukiendelea.