MAREKANI-USALAMA-USAFIRI

Donald Trump: Naridhishwa na uamuzi wa mahakama

Rais Donald Trump anakaribisha ushindi wa "usalama wa taifa".
Rais Donald Trump anakaribisha ushindi wa "usalama wa taifa". REUTERS/Carlos Barria

Rais wa Marekani Donald Trump amesema kridhishwa na uamuzi wa Mahakama ya Juu nchini Marekani kuruhusu baadhi ya Ibara za marufuku ya usafiri kwa watu kutoka nchi sita za Kiislam, viendelee kutumika.

Matangazo ya kibiashara

Bw Trump anataka kuwepo na marufuku ya siku 90 kuuia watu kutoka mataifa sita yenye Waislamu wengi wasiingie Marekani, na siku 120 dhidi ya wakimbizi.

Rais Donald trump amesema uamuzi wa mahakama sasa unaukubalia utawala wake kuzuia wageni kutoka Iran, Libya, Somalia, Sudan, Syria na Yemen, nchi ambazo anasema zina hatari kubwa sana ya ugaidi.

Mahakama ya juu zaidi ilikubali ombi la rais Donald Trump la kuruhusu sehemu ya marufuku yake dhidi ya wahamiaji kuanza kutekelezwa.

Majaji wamesema watatoa uamuzi kamili Oktoba kuhusu iwapo marufuku hiyo inafaa kudumishwa au kufutiliwa mbali.