MAREKANI

Agizo la Trump kuhusu wakimbizi kuanza kutekelezwa

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump REUTERS/Yuri Gripas

Raia kutoka mataifa sita ya Kiislamu ambao hawana ndugu wa karibu nchini Marekani wanaanza kuzuiwa kuingia nchini humo kuanzia siku ya Alhamisi.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya Mahakama ya Juu wiki hii kuamua kuwa agizo la rais Trump kuwazuia raia na wakimbizi kutoka Syria, Sudan, Iran, Somalia, Libya na Yemen kutoingia nchini humo kwa sababu za kiusalama, linaweza kutekelezwa kwa kiasi.

Rais Trump amesema hatua hiyo ya Mahakama ni ushindi mkubwa kwa taifa hilo katika jitihada zake za kuimarisha usalama wake.

Mahakama itaanza kusikiliza kesi ya kupinga agizo hilo la rais Trump mwezi Oktoba, na kufikia uamuzi wa mwisho.

Ikiwa Mahakama itaidhinisha agizo hilo, raia kutoka mataifa hayo watazuiwa kuingia nchini Marekani kwa muda wa siku 90 huku wakimbizi wakizuiwa wka siku 120.

Mataifa yaliyolengwa yamelaani hatua hiyo ya rais Trump na kusema ni kitendo cha ubaguzi.