MAREKANI-USALAMA

Marekani: Tunachunguza shambulio la mtandao linaloendelea duniani

Marekani imeanza uchunguzi kuhusu shambulio kubwa linaloendelea kiuathiri makumpuni na taasisi mbalimbali mengi duniani.
Marekani imeanza uchunguzi kuhusu shambulio kubwa linaloendelea kiuathiri makumpuni na taasisi mbalimbali mengi duniani. REUTERS/Kacper Pempel

Serikali ya Marekani imetangaza kwamba inachunguza shambulio kubwa la kimtandao ambalo limekumba mifumo ya kompyuta duniani kote wiki hii. Shambulio hilo la kimtandao lilianza nchini Ukraine na linaendelea sehemu mbalimbali duniani.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika mbalimbali ikiwa ni pamoja na taasisi za kifedha, idara za serikali, makampuni makubwa, na kampuni za usafirishaji ni ziliathirika katika shambulio hilo.

Wakati huo huo watumiaji wa mitandao mbalimbali wameambiwa kompyuta zao zimenasa mpaka walipe kiasi cha dola mia tatu katika akaunti isiyofahamika.

Wizara ya mambo ya ndani ya Marekani metahadhari na kuwashauri watu wasilipe fedha hizo, ikibaini kwamba haina uhakika kwamba, mafaili yaliyofungwa yatafunguka baada ya malipo hayo kufanyika.

Baraza la Taifa la Usalama jijini Washington limesema Marekani imedhamiria kuwachukulia hatua wahusika wa uhalifu huo wa mtandaoni.