MAREKANI-USAFIRI-WAHAMIAJI

Sheria mpya za usafiri kuanza kutumika Marekani

Maandamano dhidi ya agizo la Trump mbele ya  uwanja wa ndege wa JFK mjini New York mwezi Januari 2017.
Maandamano dhidi ya agizo la Trump mbele ya uwanja wa ndege wa JFK mjini New York mwezi Januari 2017. REUTERS/Stephen Yang

Agizo la uhamiaji la Donald Trump linaanza kutekelezwa kwa shemu moja Alhamisi hii Juni 29, 2017, kwa mujibu wa taarifa ya iliotowa siku ya Jumatatu na Mahakama Kuu.

Matangazo ya kibiashara

Raia kutoka nchi sita za Kiislamu, Syria, Iran, Yemen, Sudan, Libya, Somalia, hawawezi kupata visa ya Marekani, kama hawatoweza kuthibitisha mahusiano ya familia zao, au mtu wanaohusiana ama ushirikiano wa kibiashara na Marekani.

Hatua hiyo inayoyahusisha mataifa yalio na Waislamu kama vile Iran, Libya,Somalia,Sudan ,syria na Yemen imeangaziwa katika ujumbe uliotumwa katika balozi zote.

Baada ya miezi kadhaa ya utata na kesi mbalimbali, agizo la uhamiaji la utawala waTrump linaanza kutumika Alhamisi hii Juni 29 Kulingana na taarifa ya Mahakama Kuu, watu ambao wana uhusiano " wa nia njema" na Marekani, wanaweza kuingia nchini humo.

Jumuiya ya Waislamu nchini Marekani CAIR, ambayo ni sehemu ya walalamikaji wanaopinga agizo la utawala wa Trump kuhusu raia kutoka nchi sita za Kiislamu imesema ina wasiwasi. Wakili Gadeir Abbas anaamini kwamba umamzi wa Mahakama Kuu,una mapungufu, kwa kuweza kutafsiri sheria zihusuzo mipaka ya Marekani. "Uamuzi huu, si wa kweli, Mahakama Kuu inatumia maneno ambayo hayapo katika sheria za Marekani. Kwa kweli, watu wasio na uhusiano thabiti na Marekani, ndio ambao watapata ugumu zaidi kwa kupata visa. "

"Waislamu wote wa Marekani wana wasiwasi na uamuzi wa Mahakama Kuu, Waislamu wote ambao wana nia ya kuja Marekani wana wasiwasi na uamuzi huu, amesema Bw Abbas. Mamia ya maelfu ya watu ambao kila mwaka wanakuja Marekani kwa kuzuru DisneyWorld au kutembelea mji mkuu, wanatishiwa na uamuzi wa Mahakama Kuu. "

"Hakuna mfumo wa unaotaja kama uhusiano wa" nia njema" na Marekani, upo au la. Itakuwa kwa uamuzi wa maafisa wa polisi mpaka. Agizo la Trump linakuja kuwapa nguvu vikosi vya ulinzi kwenye mipaka ya Marekani kwa kuwakandamiza Waislamu, "ameongeza wakili Gadeir Abbas. "