MAREKANI-USAFIRI-WAKIMBIZI

Sheria ya Trump kuhusu uhamiaji yaanza kutumika

Waandamanaji wakipinga agizo la Donald Trump linalopiga marufuku raia kutoka nchi sita za Kiislamu kuingi Marekani, Januari 29, 2017 Washington DC.
Waandamanaji wakipinga agizo la Donald Trump linalopiga marufuku raia kutoka nchi sita za Kiislamu kuingi Marekani, Januari 29, 2017 Washington DC. REUTERS/Aaron P. Bernstein

Sheria ya rais wa Marekani kuhusu uhamiaji na usafiri kwenda Marekani kwa raia kutoka nchi sita za Kiislamu imeanza kutekelezwa leo Ijumaa saa sita usiku (00:00). Kwa sasa raia kutoka mataifa hayo sita ya Kiislamu na wakimbizi wote wanakabiliwa na masharti magumu ya kuingia nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Kulinagana na sheria hii mpya ya usafiri nchini Marekani, Bibi, shangazi, mjomba, binamu na mpwa hawakubaliki kuwa watu wenye uhusiano wa karibu na mtu anayetaka kuingia taifa hilo.

Sheria hii inamaanisha kwamba watu wasio na uhusiano wa karibu na wale wanaoishi nchini Marekani ama uhusiano wa kibiashara nchini Marekani huenda wakanyimwa visa na kuzuiliwa kuingia nchini humo.

Kwa mujibu wa sheria hiyo mpya, katika kipindi cha siku 90 zijazo raia kutoka mataifa hayo sita wasio na uhusiano wa karibu na raia wa Marekani hawataruhusiwa kuingia nchini humo.

Kulingana na sheria hii mpya, Wale walio na Visa hawataathiriwa.Wale wenye uraia wa mataifa mawili wanaotumia pasipoti zao pia wataruhusiwa.

Awali Jimbo la Hawaii liilishutumu serikali ya Marekani kwa kukiuka sheria ya mahakama ya juu kupitia kuwatenga watu.

Mapema juma hili, mahakama ya juu ilikubali sheria ya Trump kuhusu usafiri kutumika kwa muda.

Mahakama iliamuru kwamba watu wanaotafuta visa kuingia Marekani kutoka mataifa sita ya Kiislamu pamoja na wakimbizi wote, watalazimika kuthibitisha kuwa na uhusiano wa karibu na raia wa taifa hilo.

Mahakama ya juu inatarajiwa kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu marufuku hiyo mnamo mwezi Oktoba mwaka huu.