MAREKANI-VENEZUELA-VIKWAZO

Marekani yaiwekea vikwazo vipya Venezuela

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Agosti 6, 2017.
Rais wa Venezuela Nicolas Maduro, Agosti 6, 2017. Miraflores Palace/Handout via REUTERS

Marekani inaendelea kuiwekea vikwazo Venezuela, ambapo serikali inakabiliwa na mgogoro mkubwa wa kisiasa, ikijaribu kudhibiti taasisimbalimbali.

Matangazo ya kibiashara

Wakati ambapo maandamano yalikuwa yakiendelea katika mitaa mbalimbali, huku upinzani ukidhibi Bunge, Rais Nicolas Maduro alichukua uamuzi wa kuunda Bunge la Katiba ambalo litamruhusu kubakia madarakani baada.

Sehemu kubwa ya jumuiya ya kimataifa imekosoa mpango huo, na Washington tayari tangu kabla ya uchaguzi huo ilimuwekea vikwazo vya kisheria na kifedha Rais Maduro, na kumwita "dikteta".

Siku ya Jumatano Agosti 10, Marekani imechukua hatua mpya dhidi maafisa wanane wa serikali ya Venezuela, ikiwa ni pamoja na kaka wa aliyekua rais wa nchi hiyo Hugo Chavez. Hugo Chavez alitawala nchi hiyo toka 1999 hadi 2013.

Mabaraza mawili ya Bung hatimaye yanagongana nchini Venezuela, huku yakiendesha shughuli zao katika jengo moja la serikali. marekani tayari imeonyesha msimamo wake. Hivi karibuni Waziri wa Faedha wa Marekani alielezea utayari wa nchi yake ya kuunga mkono upinzani ambao unapambana dhidi ya dhuluma," na kwa sasa,Marekani imechukua vikwazo vinavyowalenga maafisa wanane wa serikali ya Venezuela, kwa minajili ya kusalimu amri.

Majina mapya manane yamewekwa kwenye orodha ya watu waliowekewa vikwazo na Marekani na kupiga marufuku wananchi wa Marekani kuendesha shughuli za kibiashara na maafisa hao. Miongoni mwao, mi nduguye Hugo Chavez, shujaa wa Mapinduzi ya miaka 2000, ambapo Rais Nicolas Maduro ni mrithi.