MAREKANI-KOREA KASKAZINI-USALAMA

Marekani yapuuzia vitisho vya Korea Kaskazini

Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson.
Waziri wa Mashauriano ya Kigeni wa Marekani Rex Tillerson. REUTERS/Kevin Lamarque/File Photo

Marekani kuptia Waziri wake wa Mambo ya Nje Rex Tillerson, imesema haina wasiwasi na vitisho vya Korea Kaskazini kukishambulia kisiwa chake cha Guam.

Matangazo ya kibiashara

Mapema wiki hii rais wa Marekani Donald Trump aliitishia Korea Kaskzini kwamba ataikabili kivita.

Rais Trump alijigamba katika mtandao wa Twitter kuhusu uwezo mkubwa wa zana za kinyuklia za Marekani.

“Silaha za kinyuklia za Marekani zimeimarika zaidi ya ilivyokuwa ,lakini ninatumai sitotalazimishwa kuutumia uwezo huo” amesema Donald Trump.

Tayari vita vya maneno vinaendelea kati ya nchi hizi mbili hasimu, huku wakazi wa kisiwa cha Guam wakiwa na wasiwasi ya kushambuliwa na Korea Kaskazini licha ya viongozi wa Marekani kuwatuliza nyoyo.

Hata hivyo Korea Kaskazini imeapa kukishambulia kisiwa hicho hivi karibu, kama Marekani itaendelea chokochoko zake dhidi yake.