HAITI-MAREKANI-TABIA NCHI

Kimbunga Irma kupiga katika eneo la Caribbean

Kimbunga Irmakinatarajia kupiga katika Jamhuri ya Dominika, Haiti na Cuba.
Kimbunga Irmakinatarajia kupiga katika Jamhuri ya Dominika, Haiti na Cuba. REUTERS/Ricardo Rojas

Kimbunga chenye nguvu zaidi kwa mwongo mmoja kinatarajia kupiga katika eneo la Caribbean. Kimbunga hiki kinatarajiwa kupiga visiwa vya Leeward kabla ya kuelekea Puerto Rico, Haiti na Floirda.

Matangazo ya kibiashara

Wakazi wa visiwa vilivyo eneo la Caribbean wamekua wakifanya maandalizi ya mwisho ya kuwasili kimbunga Irma.

Maafisa wameonya kuwa kimbunga Irma kinaweza kuwa chenye madhara makubwa.

Kimbunga hiki kimepata nguvu ya upepo wa kasi ya hadi kilomita 295 kwa saa.

Watu wametakiwa kuondoka katika eneo la magharibi mwa Florida.

Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza hali ya tahadhari huko Florida, Puerto Rico ba visiwa vya Virgin na kutangaza mikakati ya kukabiliana na majanga sehemu hizo.

Viwanja vya ndege vimefungwa kwenye visiwa kadhaa, maeneo maarufu ya burudani na mamlaka zimewataka watu kuenda maeneo salama.

Safari zote za ndege zimesitishwa, huku wageni wakitakiwa kuondoka Jumatano hii asubuhi na wenyeji wakitakiwa kunodoka ifikapo jioni.

Nchini Haiti, serikali imesema haina uwezo wa kulinda raia wake dhidi ya kimbunga Irma.