Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Kimbunga hatari Maria kupiga visiwa vya Caribbean

Onyo kali latolewa Martinique na Guadeloupe kabla ya kuwasili kwa kimbunga Maria.
Onyo kali latolewa Martinique na Guadeloupe kabla ya kuwasili kwa kimbunga Maria. AFP/Helene Valenzuela
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Kimbuga kipya kilichopewa jina la Maria, kinatarajiwa kuleta uharibu mkubwa katika visiwa vya eneo la Carribbean.

Matangazo ya kibiashara

Watalaam wa hali ya hewa wanasema kuwa kimbuga Maria kinatarajiwa kuleta madhara makubwa hasa katika Kisiwa cha Leewards.

Taasisi ya Marekani inayoshughulikia majanga ya kumbuga imetangaza kuwa kimbuga hiki kitatokea ndani ya saa 48 zijazo.

Onyo limetolewa katika visiwa vya Guadeloupe, Dominica, St Kitts na Nevis.

Visiwa vingine ambavyo vinatarajiwa kuathirika ni Montserrat na Martinique.

Onyo hili limekuja wakati huu, watu wakiendelea kuhesabu hasara baada ya kimbuga cha Irma katika visiwa hivyo kilichosababisha watu 37 kupoteza maisha kwa kipindi cha wiki moja iliyopita.

Ufaransa, Uingereza na Uholanzi mataifa yanayosimiamia visiwa hivyo, yameshtumiwa kwa kutofanya vya kutosha kuwaisadia watu walioathiriwa na kimbuga kilichopita.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.