Pata taarifa kuu
CARIBBEAN-HALI YA HEWA

Visiwa vya Caribbean kukumbwa na kimbunga kingine kikubwa

Kimbunga hatari Maria kinakaribia visiwa vya Leeward katika eneo la Caribbean.
Kimbunga hatari Maria kinakaribia visiwa vya Leeward katika eneo la Caribbean. Courtesy NASA/Handout via REUTERS
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Eneo la Caribbea linajiandaa kukumbwa na kimbunga kingne kikubwa kinachojulikana kwa jina la Maria. Kimbunga hiki kinatarajiwa kuwa kibunga hatari wakati huu kikikaribia visiwa vya Leeward katika eneo la Caribbean.

Matangazo ya kibiashara

Tahadhari ya kimbunga kwa sasa inachukuliwa nchini Marekani na visiwa vya Uingereza vya Virgin, St Martin, St Barts, Saba, St Eustatius na Anguilla.

Kimbunga hicho cha kiwango cha kwanza kitapata nguvu kwa haraka ndani ya saa 48 zinazokuja na kugonga visiwa hivyo baadaye leo Jumatatu.

Kwa mujibu wa utabiri wa kwanza kimbunga Maria kitapitia visiwa vya Leeward baadaye Jumatatu na Jumatatu usiku kisha kielekee maeneo ya kusini mashariki mwa bahari ya Caribbean siku ya Jumanne na Jumanne usiku.

Onyo la kimbunga limetolewa maeneo ya Guadeloupe, Dominica, St Kitts na Nevis, Montserrat na Martinique.

Baadhi ya visiwa hivyo bado vinajaribu kurejea hali ya kawadia baada ya kupigwa na kimbunga cha kiwango cha tano, kilichosababisha vifo vya takriban watu 37 na hasara ya mabilioni ya dola.

Itakumbukwa kwamba Iimbunga Irma kilisababisha uharibifu mkubwa katika visiwa vya Karibbean, hasa katika visiwa vinavyomilikia na Ufaransa na katika jimbo la Florida nchini Marekani, ambapo watu kadhaa walipoteza maisha.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.