Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

NHC: Kimbunga Maria kimekua kimbunga cha kiwango cha juu

Kimbunga Maria kwenye anga ya West Indies, Septemba 19, Kituo cha Marekani kinachoshughulika na masuala ya vimbunga.
Kimbunga Maria kwenye anga ya West Indies, Septemba 19, Kituo cha Marekani kinachoshughulika na masuala ya vimbunga. @NHC-Atlantic
Ujumbe kutoka: RFI
2 Dakika

Guadeloupe na Martinique ziko chini ya tahadhari "kubwa", ya kiwango cha juu wakati ambapo kimbunga Maria tayari kimeshambulia Jamhuri ya Dominika.

Matangazo ya kibiashara

Kimbunga Maria sasa kimefikia kiwango cha 5 (kiwango cha juu) ndani ya kipindi kisiyozidi wiki moja baada kutokea kimbunga kingine Irma kilichosababisha vifo vya zaidi ya 50 na uharibifu mkubwa katika visiwa vya Caribbean, hasa kwenye visiwa vinavyomilikiwa na Ufaransa vya Saint-Martin, Saint-Barthélemy na nchini Cuba.

Kimbunga Maria kimeendelea kukua, na kuwa kimbunga cha kiwango cha 5 siku ya Jumatatu jioni "uwezekano wa janga", shirika la Marekani linayojihusisha na masuala ya vimbunga (NHC) imebaini katika taarifa yake ya usiku wa manane. Kimbunga Maria kilifikia kiwango cha juu kwenye ngazi ya Saffir-Simpsom kikiwa na upepo unaokwenda kilomita 260 kwa saa na kutishia eneo la Caribbean.

Kimbunga Maria, ambacho tayari kimepita kaskazini mwa Martinique, kimepiga Jamhuri ya Dominika na kinatarajiwa kupiga muda si mrefu visiwa vya Guadeloupe na St Martin.

Hali ya tahadhari

Martinique na Guadeloupe ziko chini ya tahadhari ya juu. Katika Guadeloupe, Mkuu wa eneo hilo ameamuru watu kuondoka katika maeneo yaliyo hatari ya kisiwa hicho. Visiwa vya St Martin na St Barthelemy vimewekwa katika hali ya tahadhari ya juu (tahadhari nyekundu).

Ramani ya arc Caribbean kwenye tovuti ya Kituo cha Marekani kinachoshughulika na masuala ya vimbunga, Septemba 19, 2017.
Ramani ya arc Caribbean kwenye tovuti ya Kituo cha Marekani kinachoshughulika na masuala ya vimbunga, Septemba 19, 2017. http://www.nhc.noaa.gov

 

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.