MEXICO-TABIA CHI

Matumaini ya kuwapata watu wakiwa hai Mexico yafifia

Maafisa wa uokoaji nchini Mexico wamesema matumaini ya kuwapata watu hasa watoto wa shule waliokwama ndani ya vifusi baada ya tetemeko la ardhi siku ya Jumanne yamefifia.

Wasiwasi unaongezeka juu ya hatima ya watoto wa shule ya Enrique Rebsamen ya Mexico City.
Wasiwasi unaongezeka juu ya hatima ya watoto wa shule ya Enrique Rebsamen ya Mexico City. REUTERS/Edgard Garrido
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa takribani watu 300 wamepoteza maisha, huku maafisa hao wakisema kuwa kuna msichana wa miaka 12 ambaye bado yupo hai, amefunikwa na meza lakini ni vigumu kumfikia na kumwokoa.

Inaarifiwa kuwa Kimbunga Maria kimekata umeme katika kisiwa chote cha Puerto Rico, chenye watu milioni 3.5. Abner Gómez, ambaye ni mkuu wa utoaji huduma za dharura alisema kuwa hakuna mtu anayetumia umeme aliye na huduma hiyo kwa sasa.

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa 7.1 kwenye kiwango cha Richter, ambapo kina chake kinapatikana kilomita 130 kusini-mashariki mwa mji mkuu, lilisababisha majengo 50 kuporomoka katika nchi hiyo yenye watu milioni 20. Siku moja baada ya tetemeko lenye nguvu, la pili kwa wiki mbili, zoezi la uokoaji likisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea linaendelea ili kupata haraka iwezekanavyo manusura.

Kila dakika inayopita, wasiwasi unaongezeka juu ya hatima ya watoto wa shule ya Enrique Rebsamen ya Mexico City. Watoto ishirini na mmoja walikufa.

Wafanyakazi wa majanga ya dharura na wale wa kujitolewa wamekuwa wakichimbua vifusi kwa kutumia mikono.

Kuna hofu ya watoto zaidi kufariki kutokana na kwamba walikuwa darasani jengo liliporomoka.