Pata taarifa kuu
MAREKANI-TABIA NCHI

Puerto Rico: Bado tunasubiri msaada kutoka Marekani

Donald Trump ashtimiwa kutotekeleza ahadi yake ya kutoa msaada kwa kisiwa cha Purto Rico kilichokumbwa na kimbunga Maria.
Donald Trump ashtimiwa kutotekeleza ahadi yake ya kutoa msaada kwa kisiwa cha Purto Rico kilichokumbwa na kimbunga Maria. REUTERS/Jonathan Ernst
Ujumbe kutoka: RFI
Dakika 2

Serikali ya Puerto Rico inasema Marekani haijatuma usaidizi wa kutosha kuisaidia baada ya kukumbwa na kimbuga kinachofahamika kama Maria.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, serikali ya Trump imesema imefanya inachoweza kuwasaidia watu wa Kisiwa hicho kilicho na watu Milioni 3.4.

Marekani imesema imatoa Dola za Marekani Milioni 6.7 kuwasaidia waathiriwa na kimbuga hicho.

Mapema wiki hii, Rais wa Marekani Donald Trump alisema anapanga kuzuru Puerto Rico wiki ijayo ili kufuta shutma kuhusu kujikokota kwa misaada iliyotolewa na utawala wake kwenye eneo hilo linalomilikiwa na Marekani lililoharibiwa na kimbunga Maria.

Rais Trump alikutana na Ricardo Rossello, gavana wa Puerto Rico, siku ya Jumanne na kumuahidi kuwa "msaada utaendelea kutolewa" kutoka serikali ya shirikisho.

Bw. Trump alistumiwa kuwapuuzia wakazi milioni 3.4 wa kisiwa hiki kama raia wa eneo la pili, wakati ambapo wakazi wa Puerto Rico wana urai wa Marekani, hata kama hawana haki ya kupiga kura. Kwa mujibu wa wakosoaji wake, misaada ya serikali ya Marekani iliharakishwa katika majimbo ya Texas na Florida, yaliyoathirika wakati huo na vimbunga Harvey na Irma mwishoni mwa mwezi Agosti na mapema mwezi Septemba mwaka huu.

Wiki moja baada ya kupita kwa kimbunga Maria, misaada inawasili kwa kiwango kidogo katika kisiwa cha Puerto Rico, ambacho kinakabiliwa na ukosefu wa maji ya kunywa, umeme au mafuta. Shughuli za kusafisha pia zinajikokota kuanza.

"Ni vigumu sana, kwa sababu kila kitu kinapimwa. Hata kuwa na mfuko wa mchele ni vigumu," mkazi wa Bayamon (kaskazini mashariki mwa Puerto Rico) ameliambia shirika la habari la AFP.

Kwa mujibu wa mamlaka, watu 11,437 walikuwa bado wamehifadhiwa katika majengo ya serikali. Tangu siku ya Jumatatu jioni, malori 150 yaliyojaa mafuta yalisambaza mafuta hayo kwenye vituo mbalimbali vya mafuta. Asilimia 42 ya wa kazi wa kisiwa hicho hawana maji ya kunywa na hospitali 21 tu kwa jumla ya 69 ndizo zinahudumu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.