MAREKANI-TABIA NCHI

Trump aomba dola bilioni 29 kwa ajili ya waathirika wa vimbunga

Rais wa Marekani ataka waatiriwa wa vimbunga wapewe msaada wa kutosha.
Rais wa Marekani ataka waatiriwa wa vimbunga wapewe msaada wa kutosha. REUTERS/Joshua Roberts

Utawala wa Trump umeomba bunge la Congress la Marekani kupitisha mpango wa msaada wa dola bilioni 29 kwa waathirika wa vimbunga huko Texas, Florida na Puerto Rico.

Matangazo ya kibiashara

Mpango huo unajumuisha upya fedha dola bilioni 12.8 kwa waathirika wa vimbunga na dola bilioni 16 kwa mpango wa bima ya majanga ya asili.

Bahasha ya tatu ya dola milioni 576.5 (sawa na euro milioni 490.2) imetengwa kwa mikoa ya magharibi ya Marekani iliyokumbwa katika majira ya joto na visa vya moto mkubwa.

Wakati huo huo, mkurugenzi wa bajeti ya White House, Mick Mulvaney, siku ya Jumatano alihimiza mashirika ya shirikisho kuchunguza hadi Oktoba 25 mahitaji ya ziada kwa upande wa "ujenzi wa muda mrefu baada ya majanga ya asili ya hivi karibuni".

Kwa mujibu wa White House, fedha zilizoombwa siku ya Jumatano kwa bunge la Congress zitasaidia kuhakikisha msaada kwa mikoa iliyoathiriwa hadi Desemba 31. Programu hii ilikua ilitenga wiki dola bilioni 10 kutoka hazina ta serikali.

White imetenga dola milioni200 kila siku kwa msaada wa ujenzi.

Mpango wa taifa wa bima didi ya mafuriko, ambayo inalinda karibu familia milioni tano na makampuni, unadaiwa dola bilioni 16, deni ambalo White House imeaahidi kufuta, huku ikirekebisha hali ya sera ya bima.