Chama cha Democrat chapata ushindi katika uchaguzi Marekani

Mgombea wa chama cha Democrat Ralph Northam, Fairfax, wakati wa ushindi wake kkwenye kiti cha meya wa Virginia, Novemba 7, 2017.
Mgombea wa chama cha Democrat Ralph Northam, Fairfax, wakati wa ushindi wake kkwenye kiti cha meya wa Virginia, Novemba 7, 2017. REUTERS/Aaron P. Bernstein

Mwaka mmoja baada ya kushindwa kwa Hillary Clinton, chama cha democrat sasa kimeanza kuinua kichwa. Siku ya Jumanne, Novemba 7 ilikuwa siku ya uchaguzi nchini Marekani, uchaguzi muhimu tangu ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Katika tukio la uchaguzi wa ndani, chama cha Democrat kimerudi kuinua kichwa, baada ya kushinda katika uchaguzi mdogo katika mji wa New York. Mgombea wa chama cha Democrat ambaye ndio meya wa mji huo Bill de Blasio alihifadhi kiti chake.

New Jersey sasa inaongozwa na gavana kutoka chama cha Democrat. Chama cha Democrat kinatarajiwa kuhifadhi kiti hicho katika mji wa Virginia baada ya ushindani mkali unaofananishwa na ule wa uchaguzi mkuu wa Marekani uliopita.

Rais Donald Trump, ambaye alichaguliwa mwaka mmoja uliopita alikua na imani kuwa mgombea kutoka chama chake cha Republican angelishinda katika jimbo hilo muhimu.

Mjini New Jersey, mgombea wa Democrat Phil Murphy anatarajiwa kuibuka mshindi ili kumrithi Gavana asiyependwa Chris Christie.

Wapiga kura wa Virginia walimchagua mbunge wao wa kwanza katika eneo la Danica Roem.

Wapiga kura wa Virginia waliweka historia kwa kumchagua mbunge huyo aliyebadili jinsia.